Deuteronomy 5:22-27

22 aHizi ndizo amri alizozitangaza Bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.

Uoga Wa Watu Mlimani

(Kutoka 20:18-21)

23 bMliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 24 cNanyi mkasema, “Bwana Mwenyezi Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 25 dLakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu wetu zaidi. 26 eNi mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 27 fSogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mwenyezi Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mwenyezi Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

Copyright information for SwhKC